VIGOGO 111 wanaosadikiwa kujihusisha na biashara yharamu ya madawa ya kulevya nchini wameanza kuonja 'joto ya jiwe' kufuatia Jeshi la Polisi Tanzania Kitengo cha Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola kukamata mali zao, Uwazi lina mpango mzima.
Kamanda Nzowa.
Kuhusu mali ambazo ni magari, ilidaiwa kuwa kufuatia taarifa zilizowataja wauza unga, jeshi la polisi liliamua kushikilia magari hayo na kufanya uchunguzi wa uhalali wake.
“Kuna watu walitajwa majina, wakafuatiliwa, magari yao yakakamatwa na kufanyiwa uchunguzi, lakini cha kushangaza baadhi yao wameingia mitini na kutelekeza magari yao,” kilisema chanzo.
Chanzo kilisema baadhi ya magari hayo ni Mercedes Benz, Jeep, Toyota Spacio, Toyota Galsira, Toyota Mark II, Nissan Patrol 4x4 GL, Toyota Land Cruiser na Toyota Prado.
Uwazi lilifanikiwa kunasa majina ya vigogo waliokamatwa wakiwa na unga na kiasi walichokamatwa nacho.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili katika mahakama mbalimbali nchini na ndani ya jeshi la polisi umebaini kuwa, kesi za watuhumiwa hao zinaendelea kuunguruma kortini japokuwa kasi yake si ya kuridhisha.
POLISI WABUNI MBINU MPYA
Vyanzo hivyo viliendelea kudai kwamba polisi wamebuni mbinu mpya ya kuwakamata vigogo wa madawa ya kulevya wakiamini itawapa mafanikio zaidi.
“Siku hizi si kama zamani, jeshi la polisi tumebuni mbinu mpya ya kuwakamata hawa jamaa (vigogo). Mbinu hii italeta mafanikio makubwa zaidi,” alisema mtoa habari wetu.
WAPAMBANAJI WA UNGA HATARINI
Taarifa zaidi zinadai kwamba usalama wa viongozi wanaopambana na wahusika wa unga nchini upo shakani kutokana na vitisho vinavyotolewa na mtandao huo duniani kote.
Inaaminika kuwa wengi wanaopambana au kupiga vita madawa ya kulevya, hususan viongozi na waandishi wa habari, hutendwa vibaya wakati mwingine kuuawa kabisa.
UWAZI LAMSAKA KAMANDA NZOWA
Kufuatia taarifa hizo za kiuchunguzi, katikati ya wiki iliyopita, mapaparazi wetu walimtafuta Kamanda wa Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa na kumuuliza kuhusu zoezi zima la kamatakamata ya wanamtandao hao.
Kamanda Nzowa alisema zoezi la kuwakamata wanaojihusisha na biashara hiyo linaendelea vizuri.
Alisema mpaka Mei, mwaka huu kikosi chake kimeshakamata kiasi kikubwa cha unga na kuongeza kuwa anaamini kasi ya biashara hiyo nchini imepungua sana.
Aliongeza kuwa askari wake wamejipanga vizuri na wana mafunzo maalum ya kuwatambua watu hao hatari.
VIGOGO HUWALISHA KIAPO KIBAYA WANAOWABEBESHA
“Tumewakamata ‘mapapa’ (wauza unga wadogo) wengi sana na tunahakikisha kwamba ‘nyangumi’ (wauza unga vigogo) nao hawachomoki.
“Mara nyingi vigogo wamekuwa wakiwalisha kiapo kibaya vijana wanaowabebesha unga kwamba ikitokea wakakamatwa wasiwataje lakini nao tunawabana kitaalam mpaka wanawataja, kwa sasa bado tunaendelea kuwadaka,” alisema Kamanda Nzowa.
Kamanda huyo aliwataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi lake dhidi ya wauza madawa ili kutokomeza kabisa biashara hiyo.
ULINZI VIWANJA VYA NDEGE NCHINI SASA NI MOTO
Katika maongezi yake, Afande Nzowa alisema ulinzi umeimarishwa katika viwanja vya ndege, bandarini, mipaka ya nchi na sehemu zote zinazohisiwa kuweza kupitishwa madawa hayo.
AANIKA MAJINA 111
Kamanda Nzowa alikwenda mbele zaidi kwa kuweka wazi takwimu ya ukamataji wa watuhumiwa hao kutoka mwaka 2009 hadi Mei, 2013.
Orodha chini inabainisha kiasi na aina ya madawa waliyokamatwa nayo katika mabano.
Steven Gwaza, (heroin gramu 825.7), Rebecca Wairimu Mwangi (heroin gram 1,800), Khatibu Bakari Khatibu, Khalid Salim Maunga, (cocaine gramu 1,007.4), Dhoulkefly Awadh, (cocaine gramu 893.58), Abdallah Pashua Kipevu (heroin gramu 31,000), Diaka Brama Kaba (heroin gramu 31,000), huyu alikamatwa akiwa na Ndjane Abubakar, Sylivia Kaaya Namirembe, Farid Kisuule, Robinson Dumba Teise na Ismail Mugabi.
Wengine ni Rashid Salim Mohamed, (cocaine gramu 1,374.32), Mini Thabo Hamza (cocaine gramu 1,595.74), Hamis Mohamed Mtou (cocaine gramu 850), Kwako Sarfo, Mnigeria (cocaine gramu 1,1951.80), Mustapha Musa (cocaine gramu 286), alikuwa na Aman Saidfadhil Daruweshi na Afshin Jalal.
Kamanda Nzowa akaendelea kuwaanika, Jack Vuyo, (heroin gramu 42,000) huyu alikuwa na Anastazia Elizabeth Cloete. Simon Eugenio Fadu (cocaine gramu 8,000), Assad Aziz, (heroin gramu 50,000), alikuwa na Isamil Shebe Ismail, Rashid Salim na Majed Gholamghader.
Wengine kwenye orodha hiyo ni, Anna Jamaniste Mboya, (cocaine gramu 1,140), Fredy William Chonde (heroin gramu 175,000), Kambi Zuber, Abdul Ghan na Shahbaz Malik, Livinus Malik (Wapakistani) (cocaine gramu 804.7), Chukwudu Denis Okechukwu, Paulo Ekechukwu na Hycenth Stan (Wanigeria) (cocaine gramu 81,000).
Aidha wapo, Shoaib S.O. Mohammed, Fedro Alfredo Chongo, (cocaine gramu 1,530), Kadiria Said Kimaro (heroin gramu 1,365.91), Abdallah Rajab Mwalimu (cocaine gramu 716.5), Mwiteka Godfrey Mwandemele (cocaine gramu 1,112), Abbas Kondo Gede (cocaine gramu 1,112), Mwanaidi Ramadhan Mfundo (cocaiane gramu 5,000), alikuwa na Sarah David Munuo, Antony Karanja, Benny Ngare, Almasi Hamis Said, Yahya Haroun Ibrahim, Aisha Said Kungwi, Rajab Juma Mzome na John William Mwakalasya.
Wengine ni Ally Mirzai Pirbakhshi (cocaine gramu 97,000) alikuwa na Aziz Juma Kizingiti, Said Mashaka Mrisho, Abdulahman Mtumwa na Hamidu Kitwana Karimu.
Ramadhan Athuman (heroin gramu 3,000) alikuwa na Rashid Mohammed, Ally Mohammed Kichaa na Issa Abdulahman. Rashid Ally Mtopea (heroin gramu 12,000) alikuwa na Idd Adam Mwaduga, Nurdin Adam. Maurine Amatus Lyumba, John Adams Igwenma wa (Mnaijeria) ( cocaine gramu 830.19).
Upendo Mohammed Cheusi, Abdallah Omar Salum (cannabis sativa gramu 1,000) alikuwa na Cosmos Chukwumezie, Ifeanyi Malven Kalu Oko (Wanaijeria) (heroin gramu 3,185.38), Allan Duller (cocaine gramu 3,882.92), Alberto Mendes kutoka Ghana, (gramu 1,277.10 za heroin)
Wengine ni Joseph Chukwumeka Nwabunwanne Minigeria, (gramu 1,245.96 za heroin) Kwaku Safo Brobbey Mghana (gramu 13,781.78 za heroin), Princewill Ejike Mnigeria (gramu 981.12 za heroin),Mary Mvula Mzambia (gramu 391.51 za cocaine), Waziri Shaban Mizongi, (gramu 2,013 za heroin) akiwa na Santos Joseph Mpondela, Kelvin Kelven Mwazeni.
Wengine ni Emmanuela Adom, Mghana (gramu 9,838.1 za cocaine), Asha Omary Ramadhan, (gramu 1.56), Mariam Mohammed Said, (gramu 9,857.54 za bangi) akiwa na Abdullatif A. Fundikira
Aliendelea kuwataja Marceline Koivogui, Mghana (gramu 1,073.82 za heroin), Edwin Cheleh Swen Mliberia (gramu 1,509.35 za heroin), akiwa na Benjamin Obioma Onuorah wa Nigeria, Sofia Seif Kingazi, (gramu 3,379.54 za cocaine), Josephine Mumbi Waithera Mkenya (gramu 3,249.82 za cocaine), Iddi Juma Mfaume,( gramu 563.25 za heroine), Amina Kassim Ramadhani,( gramu 1,980.11 za heroine) na Vivian Edigin Mnigeria ( gramu 797.56 za cocaine), Hadija Tambwe,( gramu 33,507.04 Za cannabis), Sasha Farhan na Mnyeke Sativa, na Mychel Andriand Takahindangeng Muindonesia,( gramu 3,932.44 za cocaine).
Wengine ni Kristina Biskavevskaja Mluthenia (gramu 4,000 za cocaine), Stephen Basil Ojiofor Mnigeri (gramu 1,173 za cocaine), Judith Marko Kusekwa, ( gramu 1,793 za heroin), Khamis Said Bakari,( gramu 1,793 za heroin).
Kundi la mwisho ni Tabia Omary au Neema Omary (gramu 994.97 za heroin), Masesa au Habiba Andrew Joseph, ( gramu 1,037.9 za heroin).
Hivi karibuni Agness Gerald ‘Masogange’ na mwenzake walikamatwa Afrika Kusini wakiwa na kilo 150 za dawa za kulevya.
0 komentar:
Post a Comment