MALORI YA TANZANIA YARUHUSIWA KUPITA KWA TOZO YA ZAMANI MPKANI RWANDA

Naibu Waziri wa Uchukuzi  Dk. Tzeba  amethibitisha kuwa Serikali ya Rwanda imeruhusu malori ya Tanzania yaendelee na safari kwa kulipa dola 152 badala ya 500 zilizoanza kutozwa hapo  jana.
 Akiongea  toka  mkoani  Dodoma, Tzeba  ameweka  wazi  kuwa  Waziri wa Fedha wa Rwanda  aitwaye Gatete na wa  waziri  wa  Uchukuzi wa  Rwanda aitwaye  Rwakabamba, wameridhia tozo ya dola 152 iendelee  kutumika.
Tzeba  amedai  kuwa  ofisa mmoja katika Wizara ya Fedha ya Rwanda ndiye aliyekurupuka na kutangaza mabadiliko hayo kwa mdomo.
Waziri wa Fedha wa Rwanda alipoulizwa na mwenzake wa Tanzania, alishituka  na kuahidi kulipatia ufumbuzi  tatizo  hilo ambapo  ndani ya muda  mfupi  jibu lilipatikana kuwa agizo la ofisa huyo wa Rwanda halikuwa halali. 
Mbali  na  kauli  ya  Tzeba, habari  za  CHUMBANI  ambazo  mpekuzi  wetu   amezipata  zinadai  kwamba  uamuzi huu umefikiwa  na  serikali  ya  Kagame  baada ya Mamlaka Ya Mapato Tanzania (TRA) kulazimika kupunguza ushuru wa barabara ( Road Toll) kwa magari yenye plate numbers za Rwanda  kwa  asilimia  170.
 Kwa  hali  hii, ni  dhahiri  kuwa  huu  utakuwa  ni ushindi mkubwa kwa Rwanda ikizingatiwa kuwa umbali kutoka Dar  es Salaam mpaka Rusumo ( mpakani )sio sawa na umbali kutoka Rusumo mpaka Kigali.

0 komentar:

Post a Comment

Blog Archive