SAKATA LA VIGOGO WA CHADEMA KUKAMATWA NA POLISI



Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, wabunge Tundu Lissu, Peter Msigwa, Joseph Mbilinyi (Sugu), David Silinde na viongozi wengine wa mkoa na Wilaya ya Iringa mjini, akiwemo Diwani Nyalusi, wamekamatwa  na Jeshi la Polisi, Kituo Kikuu Iringa  na  kuhojiwa  kwa  masaa  matatu.

Viongozi hao   walikamatwa  majira ya saa 3 asubuhi katikati ya mji wa Iringa wakati wakitokea eneo la Kihesa kuelekea Bungeni mjini Dodoma kwa shughuli za kibunge.
 Akithibitisha kukamatwa kwa  viongozi hao ,  kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi amesema kuwa viongozi hao walikamatwa kwa mahojiano kutokana na kutoa kauli hatarishi kwa amani ya  Tanzania wakati wa mkutano wao uliofanyika katika uwanja wa Mwembetogwa kwa ajili ya mabaraza ya ukusanyaji wa maoni ni rasmu ya katiba.

 Kamanda Mungi amesema kuwa kibali ambacho Chadema walipewa kilikuwa kikianza saa 9 Alasili hadi saa 12 :00 ila wao waliendelea na mkutano huo hadi majira ya saa 12 .25 na kila walipofuatwa zaidi ya mara moja kuelezwa kuhusu muda wa kibali chao kuisha bado viongozi hao waliendelea kuendesha mkutano huo huku wakitumia vipasa sauti kutoa maneno ya dhahaka dhidi ya jeshi la polisi.
Hata hivyo Mungi amesema kuwa jeshi la polisi lilishindwa kutumia nguvu  kuwakamata ama kuwashusha viongozi hao jukwaani wakati wa mkutano huo kama njia ya kuepusha vurugu ambazo zingeweza kutokea iwapo nguvu zingetumika kuwashusha kwa kuvunja sheria za nchi .

 "Tunawashikilia viongozi hao kutokana na kutoa kauli hatarishi wakati wa mkutano wao wa jana (juzi) uliofanyika uwanja wa Mwembetogwa ...
"Kibali chao kilikuwa kikiisha saa 12 .00 jioni ila wao walizidisha muda na maofisi wa polisi waliokuwepo waliwafuata na kuwakumbusha juu ya muda waliopewa katika kibali chao ila wao badala ya kusitisha mkutano walitumia kipasa zauti kujibu na kutoa kauli cha hatarishi ....

"Jeshi la polisi lilitumia busara na kuwaacha hadi walipomaliza na asubuhi tuliwakamata kitaalam bila ya kutokea vurugu zozote" Mungi

 Amesema kuwa viongozi hao hadi majira ya saa 5  leo  asubuhi walikuwa wakiendelea kuhojiwa na jeshi la polisi na kuwa kufikishwa ama kutofikishwa mahakamani kutajulikana mara baada ya mahojiano hayo .

 Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Iringa Suzana Mgonakulima alisema kuwa jumla ya waliokamatwa jana ni viongozi wanne akiwemo Mbowe, mbunge Msigwa , Lissu pamoja na diwani wa kata ya Mvinjeni katika Manispaa ya Iringa Frank Nyalusi .
Kuhusiana na kumamatwa na kuachiwa kwa viongozi hoa amesema kuwa viongozi hao waliachiwa majira ya saa 5.30 asubuhi baada ya kuhojiwa kwa zaidi ya masaa matatu ambapo kila mmoja alitakiwa kudhaminiwa na mtu mmoja kwa dhamana ya Tsh milioni 2 na wote walikidhi masharti ya dhamana na kuruhusiwa kuendelea na safari hadi hapo watakapotakiwa kufika polisi .

0 komentar:

Post a Comment

Blog Archive