Maandamano ya chama cha CHADEMA yaliyokua yanafanyika huko mwanza yamegeuka vurugu baada ya wandamanaji kuanza kupambana na polisi.
CHADEMA walikua wakiandamana katika kushinikiza Meya wa Ilemela Henry Matata aachie ngazi kwani hana sifa zakua meya, baada ya kuvuliwa uanachama na chama hicho.
Katika picha zilizokirushwa kupitia televisheni ya Barmedas Tv ya Mwanza, barabara zimeonekana zikiwa zimefungwa kwa mawe na miti, huku katika maeneo mengine uchafu ukiwa umejazwa barabarani na matairi kuchomwa.
katika mtaa wa Mission waandamanaji wamefunga barabara kwa uchafu uliokua katika dampo moja kando ya barabara hiyo.
Maandamoano hayo yalikua yamalizikie viwanja vya furahisha ambapo viongozi wa chadema walikua wahutubie.
Chanzo cha vurugu hizo hakijafahamika, ikizingatiwa CHADEMA walikua na kibali cha kufanya maandamano hayo.
Hivi sasa polisi wametanda mitaani katika kudhibiti vurugu hizo na hali inaonekana kutengamaa.
0 komentar:
Post a Comment