DANGULO LA MAKAHABA LAGUNDULIKA BUGURUNI


JUMBA linalodaiwa kutumika kuendesha shughuli za ukahaba limebainika kuwapo katika eneo la Buguruni, jijini Dar es Salaam.

Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima, umebaini kuwapo kwa jumba ambalo linatumika kama nyumba ya kulala wageni, ambako idadi kubwa ya makahaba hujazana na kuendesha biashara ya kuuza miili yao bila wasiwasi. 



Wasichana wanaofanya biashara hizo hutoza kiasi cha sh 5,000 kama huduma ya ngono na chumba kwa matumizi ya muda mfupi.

Biashara hiyo ambayo imeleta usumbufu mkubwa kwa wakazi wengi wanaopakana na nyumba hiyo, imekuwa

ikifanikiwa kutokana na kuwapo kwa baadhi ya askari polisi wanaodaiwa kuwalinda wasichana hao pamoja na mmiliki wa nyumba hiyo.

Nyumba hiyo inavyo vyumba vingi vinavyotozwa kiasi sha sh 1,200 kwa chumba pamoja na kondomu. Kadhalika wasichana wenye umri wa miaka 15, ni miongoni mwa wanaofanya biashara hiyo.

Mjumbe wa serikali ya mtaa wa eneo hilo, Amiri Banza, alikiri kuwapo kwa biashara hiyo, ingawa alisema wamejaribu sana kuzuia hali hiyo bila mafanikio: 
“Tumechoka na hii kadhia, tumeripoti kwa viongozi wa Kata hadi polisi lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa. Kama wakija polisi wanawakamata, halafu wanawaachia,” alisema.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi wa Ilala, Marietha Minangi alipoulizwa juu ya kuwapo kwa jumba hilo alisema hajui chochote.: “Mimi sijapata taarifa hizo na ndiyo kwanza ninakusikia wewe,” alisema.

Alipoulizwa kuhusu polisi kufika kwenye jumba hilo na kuchukua rushwa na kuondoka alisema: “Sina ushahidi, kama wapo polisi wanafanya hivyo ni kosa,” alisema Minangi na kuongeza kuwa polisi wanafanya doria maeneo hayo na mara kadhaa wamewakamata watu wanaojihusisha na vitendo hivyo na kuwafikisha mahakamani.

0 komentar:

Post a Comment

Blog Archive